Ads 468x60px

Friday, June 15, 2012

Milango Ya Mafanikio Yaanza Kufunguka Kwa DJ Fetty Baada Ya Kukamua BBA 7

Siku mbili tu za kupiga ngoma kwenye jumba la Big Brother Africa na kuoneshwa live, zimempa Dj Fetty michongo inayoweza kubadilisha maisha yake milele.

Ishu ni kwamba asubuhi tu ya jumatatu baada ya kusababisha kwenye 'moja na mbili' usiku wa jumapili, mwaliko kutoka nchini Rwanda ukatua kwa mawasiliano ambayo hajayataja!

Hilo ni moja tu, lingine ni kwamba baada ya show ambayo kiukweli aliimuudu vema ukizingatia kuwa ni DJ wa kike, wawakilishi wa kituo cha Channel O walimfuata na kumtaka kama vipi awe anapiga ngoma kwenye show yao ya Madj iitwayo Basement.

Mpaka sasa ni kwamba yupo kwenye mazungumzo na kwakuwa wao ndio waliomfuata basi uamuzi unabaki kwake tu.

Sisi tulipopata taarifa kuwa Big Brother imemchukua Fetty akapige ngoma kama DJ mwalika, tulijua tu kuwa huo unaweza kuwa mwanzo muhimu kwake kama DJ na mtangazaji wa kimataifa. Kinachomsaidia Fetty ni muonekano wake na kujiamini.

Ana muonekano wa kuvutia wenye label ya kimataifa zaidi. Ni msichana ambaye kama kweli akiamua kujifua na kukubali kuishi maisha kama DJ, sasa hivi anaweza kufikia ndoto za madj wachanga na wakubwa duniani wa kike kama Dj Diamond Cutz wa BET.

Kwa kuonekana kwake Big Brother wengi wamemmezea mate husasan vituo vya TV ukiachilia mbali Channel O.

Dj Fetty amefanikiwa kujitengeneza kama brand ambayo kituo chochote cha radio ama TV kitanufaika nayo kiumaarufu kutokana na upekee wake.

Jambo la msingi ambalo sasa hivi Dj Fetty anatakiwa kufanya kama anataka kuifufua tena career yake kama Dj wa kike tofauti na utangazaji tu, ni kujiimarisha zaidi kwenye mashine za mixing.

Anahitaji kufanya mazoezi ya ziada ili kama akianza rasmi kazi kama DJ wa kimataifa watu wamwelewe kama Dj mkali na si kama Dj wa kike mkali.
Maana yake ni kwamba, uwezo wake sasa unatakiwa kuwa mkali zaidi na kulingana walau kidogo na uwezo wa madj wakali nchini kama Tass, Stevie B, Mafuvu, Maliz na wengine.

Ni ngumu kuwa kama wao lakini kwa mazoezi na nia moja hakuna kinachoweza kushindikana.

Kingine japo muziki anaufahamu anatakiwa kuongeza ufahamu zaidi wa aina mbalimbali ya muziki kwa kufuatilia playlist ya vituo vikubwa vya radio na TV.
Kwa jinsi alivyoonesha uzuri wake katika mixing, ni muda sasa wa yeye kufikiria kuwa na meneja anayejua masuala haya hasa katika mtazamo wa kimataifa zaidi.

Hii ni kwasababu akiwa ‘too nice’ ni ngumu kupata michongo yenye hela nyingi. Mameneja siku zote hulipwa ili wasiwe too nice unapohitajika.
Hata hivyo anahitaji kuwa na mtu anayemuamini kumpa cheo hiki.

Ni matumaini yetu kuwa baada ya miaka kama miwili tu hivi, Fetty hatakuwa huyu tunayemjua leo hii. Kila lakheri Dj Fetty.

0 comments:

Post a Comment