Ads 468x60px

Wednesday, July 4, 2012

NJOMBE,

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe George Mkindo Ametolea Ufafanuzi  Suala la Ubadhirifu wa Fedha za Kijiji cha Idunda Takribani Shilingi Milioni Kumi Unaodaiwa Kufanywa  na Viongozi Waliokuwepo Madarakani , na Kusema Kuwa Suala Hilo Bado Linafanyiwa Uchunguzi na Hivyo Kuwataka Wananchi wa Kijiji Hicho Kuwa na Subira.


Amesema Kuwa Uongozi wa Halmashauri ya Mji Unaendelea Kufanya Uchunguzi Juu ya Malalamiko Hayo ya Wananchi na Mara Uchunguzi Utakapokamilika Hatua za Kisheria Zitachukuliwa Dhidi ya Viongozi Hao na Kwamba Wananchi Watajulishwa.

Akizungumzia Suala la Baadhi ya Viongozi wa Serikali ya Kijiji Hicho Kutoroka Akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji cha Idunda, Mkurugenzi Mkindo Amesema Hana Taarifa Juu ya Kutoroka Kwa Mwenyekiti Huyo Huku Akiwataka Wananchi Kutoa Malalamiko Yao Kwa Kufuata Utaratibu Kwa Kutoa Taarifa Katika Ofisi Husika Mapema Iwezekanavyo.

Ufafanuzi Huo Umekuja Kufuatia Malalamiko Yaliyotoka na Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Idunda , Kutokana na Ahadi Iliyotolewa na Uongozi wa Halmashauri ya Mji  Kwenye Mkutano wa Hadhara Kati ya Wananchi na Mkurugenzi Huyo Ambapo Wananchi Hao Waliahidiwa Kurejeshwa Fedha Hizo Mei 25 Mwaka Huu Lakini Hadi Hivi Sasa Fedha Hizo Hazijarejeshwa.


NJOMBE,

Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Wilayani Njombe Imewataka Wafanyabiashara Kuendesha Biashara Zao Kwa Kufuata Sheria Ikiwa ni Pamoja na Kulipia Kodi za Biashara Wanazoendesha Kwa Wakati Ili Kuepusha Usumbufu Kati ya Wafanyabiashara Hao na Mamlaka Hiyo.

Akiongea na Kituo Hiki Meneja wa TRA Wilayani Njombe Bwana Charles Mkumbo Amesema Mamlaka Hiyo Huwatembelea Wafanyabiashara Ambao Wamekadiriwa Malipo ya Kodi za Biashara Zao Kwa Lengo la Kufanya Ukaguzi Ili Kuthibitisha Kiwango cha Kodi Walizokadiriwa Kulingana na Biashara Wanazozifanya.

Amesema Kwa Sasa Wafanyabiashara Wengi Wamekuwa Wakilipia Biashara Zao Bila Usumbufu Ikiwa ni Pamoja na Utumiaji wa Mashine za Kimahesabu EFD, Huku Akiwataka Wafanyabiashara Hao Kuchukua Stakabadhi za Bidhaa Wanazonunua. 

Akizungumzia Mfumo wa Ulipaji Kodi za Mapato Kwa Kutumia Njia ya Simu Kama M-Pesa , Meneja Mkumbo Amesema Utaratibu Huo Kwa Mkoa wa Njombe Bado Haujaanza Kutumika na Kwamba Utaratibu Huo Unatumika Katika Miji Mikubwa Kama Dar Es Salaam na Umeanzishwa Kwa Lengo la Kuondoa Msongamano Katika Miji Hiyo Wakati wa Ulipaji Kodi.
............................................................................................................
NJOMBE,

Shirika Lisilo la Kiserikali Linalojisghulisha na Utunzaji wa Mazingira SECO Wilayani Njombe limefanikiwa Kutoa Elimu ya Kuongeza Hewa ya Ukaa Katika Vijiji Vinavyouzunguka Msitu wa Njilikwa Kwa Lengo la Kuboresha Mazingira ya Mji wa Njombe.

Akiongea na Kituo Hiki Mwenyekiti Msaidizi wa Shirika la  SECO Bwana Yohana Kondowe Amesema Kuwa Elimu hii ya Kuongeza Hewa ya Ukaa Iliyotolewa kwa Vijiji Vinavyouzunguka Msitu Huo  Ilidhaminiwa na Shirika la WWF.

Ameongeza Kuwa Baada ya Kutolewa Elimu Hiyo Wananchi wa Maeneo ya Msitu wa Njilikwa Wamekuwa na Uelewa Kwa Sababu Wameacha Kukata Miti Ovyo na Viongozi nao Wamekuwa Wakitunza Fedha Vizuri  Zinazopatikana Kutokana na Rasilimali Zilizopo  Kwenye Msitu Huo Tofauti na Zamani Ambapo Fedha Zilikuwa Zikifichwa.

Bwana Kondowe Amesema Kuwa Ilikuepuka Kuongezeka Kwa Hewa ya Ukaa Inatakiwa Itolewe Elimu kwa Wananchi  Mara Kwa Mara Kwa Njia ya Midahalo na Mikutano ya Hadhara Ili Kupunguza Tatizo Hilo.

Kutokana na Njombe Hivi Sasa Kuwa Mkoa Shirika Hilo Limejipanga Kujitangaza Kimkoa na KutoaElimu Juu ya Utunzaji wa Mazingira Ili Kuondokana na Tatizo la Uharibifu wa Mazingira na Pia  Akiweka Wazi Mpango wa Shirika Hilo wa Kutoa Elimu Katika Kata ya Igominyi Kuanzia Mwezi Septemba hadi March Mwakani.

.............................................................................................................
NJOMBE,

Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Inatarajia Kuanzisha Mashamba ya Darasa ya Ufugaji Nyuki Katika Maeneo Mbalimbali Ikiwa ni Utekelezaji wa Agizo la Mkuu wa Mkoa wa Njombe Kapteni Mstaafu Assery Msangi Alieiomba Halmashauri Hiyo Kuanza Kuhamasisha Ufugaji wa Nyuki Kama Njia Mojawapo ya Kuongeza KIpato Cha Wananchi.

Katika Mpango Huo Halmashauri Hiyo Inatarajia Kuanza na Vijiji Vya Masaulwa ,Madeke,na Mambegu Katika Kipindi Cha Mwaka wa Fedha 2012/2013 Ambapo Wanatarajia Kuzingatia Zana Bora na za Kisasa.

Afisa Uhusiano Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Bw Lukelo Mshaura Amesema Pamoja na Mpango Huo Halmashauri Hiyo Pia Imejipanga Kuanzisha Vikundi Vya Ushirika wa Wafugaji Nyuki Ambao Utasaidia Kupunguza Changamoto Mbalimbali Zinazowakabili  Kwa Kupitia Wataalam Waliopo Kwenye Maeneo Yao.

Halmashauri ya Wilaya ya Njombe ina mizinga elfu Arobaini na tatu mia tatu sitini na tano  Ikiwa ya kisasa ni mizinga  elfu tatu mia tano ishirini na tatu  Na mizinga ya kienyeji ni Elfu thelethini na tisa mia nane arobaini na mbili.

Akiwa Kwenye Ziara Yake Kwenye Halmashauri Hiyo Mkuu wa Mkoa wa Njombe Aliuagiza Uongozi wa Halmashauri Hiyo Kuhakikisha Kuwa Hadi Kufikia Mwaka 2014 Inapata Mizinga 1000 ya nyuki kama chanzo cha mapato katika halmashauri na kuiwezesha jamii kuongeza kipato chao.

.............................................................................................................

0 comments:

Post a Comment