Ads 468x60px

Thursday, July 5, 2012

NJOMBE,
 Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Limewataka Wamiliki Wote wa Silaha za Moto Kujitokeza Kwa Ajili ya Kusajili Silaha Zao Ikiwa ni Zoezi la Nchi Nzima Lililoanza Leo Wilayani Njombe. Kamanda wa Polisi Mkoani Njombe ASP Fulgency Ngonyani Amesema Zoezi Hilo Katika Wilaya ya Njombe Litadumu Kwa Siku Mbili Hadi Kesho July Tano Kabla ya Kuhamia Katika Wilaya za Ludewa na Makete Wakati Wilaya ya Wanging'ombe Wakitakiwa Kusajili Wilayani Njombe. Pia Ametoa Wito Kwa Wamiliki wa Silaha Kuzingatia Matumizi Sahihi ya Silaha Hizo Kulingana na Maelekezo Waliyopewa na Hivyo Kusaidia Kupunguza Matukio ya Uhalifu .


 NJOMBE,

 Kikundi cha Walemavu cha Nyombo Kwa Kushirikiana na Wataalam wa Afya Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Kimefanikiwa Kutoa Mafunzo ya Kujikinga na Maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi Kwa Walemavu wa Vijiji Vitatu Vya Kata za Ikuna na Ninga Mkoani Njombe. Akiongea na Kituo Hiki Mwenyekiti wa Kikundi cha Walemavu Kwa Kata za Ikuna na Ninga Bwana Thadei Mwenda Amesema Wameamua Kutoa Mafunzo Hayo Kwa Watu Wenye Ulemavu Kutokana na Jamii ya Walemavu Kutoshirikishwa Katika Masuala Mbalimbali ya Kijamii. Aidha Bw Mwenda Amesikitishwa na Tabia ya Baadhi ya Watendaji wa Serikali za Vijiji Kutowataarifu Watu Wenye Ulemvu Juu ya Masuala Yanayowahusu Hali Ambayo Inaonyesha Jinsi Watu Hao Wasivyothanika Katika Jamii. Amesema Awali Mafunzo Hayo Yalilenga Kutolewa Kwa Walemavu 178 Kutoka Kata za Ikuna na Ninga Lakini ni Walemavu 95 Ndio Waliofanikiwa Kushiriki Huku Wengine Wakishindwa Kushiriki Kutokana na Sababu Mbalimbali Ikiwemo Mawasiliano Duni Dhidi ya Viongozi Wao. Akizungumza Mara Baada ya Kumalizika Kwa Mafunzo Hayo Mganga wa Zahanati ya Nyombo Bi. Oresta Luambano Amesema Kupitia Ziara Hiyo Amebaini Changamoto Mbalimbali Zinazowakabili Walemavu Hasa Maeneo ya Vijijini Zikiwemo Huduma za Afya na Elimu na Hivyo Kuwataka Viongozi wa Serikali za Vijiji Kuondokana na Dhana Potofu Juu ya Watu Wenye Ulemavu ..................................................................................... NJOMBE; Wakati Tume ya Kukusanya Maoni ya Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba Ikiwa Imeanza Kazi Yake Rasmi Katika Mikoa Minane Hapa Nchini Huku Baadhi ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Yakitoa Elimu Juu Mabadiliko ya Katiba Hiyo, Baadhi ya Viongozi wa Dini Mjini Njombe Wamesema Bado Wananchi Wengi Hawajaelewa Mambo Ambayo Yanahitaji Kufanyiwa Mabadiliko Katika Katiba Iliyopo Sasa Miongoni Mwa Viongozi Hao ni Mchungaji wa Kanisa la Tanzania Presybterian (Amani) Mjini Njombe Bwana Zakayo Fisima Ambae Ameonyesha Wasiwasi Wake Juu ya Utoaji wa Maoni ya Mabadiliko ya Katiba Hasa Kwa Wananchi wa Maeneo ya Vijijini Kwani Hata Katiba Iliyopo Sasa Hawajawai Kuiona. Akizungumzia Suala la Vitendo Vya Uchomaji wa Makanisa Vilivyotokea Zanzibar , Mchungaji Fisima Amesema Hali Hiyo Imesababishwa na Itikadi za Kidini na Kuongeza Kuwa Jambo Hilo Linahatarisha Amani ya Nchi na Waumini wa Dini Moja na Nyingine. Katika Hatua Nyingine Mchunga Fisima Amesema Suala la Tofauti za Dini Litaendelea Kuwepo na Kwamba Misingi ya Neno la Mungu na Mahusiano Kati ya Mtu na Mtu Ndio Jambo Linalohitajika , Ambapo Amewaasa Waumini Kuheshimiana Hasa Katika Misingi ya Kiimani ya Dini. ..................................................................................... NJOMBE; Shirika la Wanawake Molimoli la Mjini Njombe Limedhamiria Kuwawezesha Wanawake na Kupunguza Wimbi la Watoto Wanaoishi Katika Mazingira Magumu Kwa Kutoa Huduma Mbalimbali za Kijamii IKiwemo Mafunzo ya Ujasiriamali. Katibu wa Shirika Hilo Bi.Malisiana Max Amesema Ili Kupunguza Tatizo la Ajira Kwa Vijana Molimoli Inatarajia Kuanzisha Shule ya Ufundi wa Kazi za Mikono na Kutoa Mafunzo ya Ujasiriamali Hali Ambayo Itasaidia Kupunguza Wimbi la Vijana Wengi Wasioa na Ajira na Wanawake Tegemezi. Bi.Max Ameelezea Baadhi ya Changamoto Zinazolikabili Shirika Hilo Kuwa ni Ukosefu wa Fedha , Kuchelewa Kupata Mikopo Wanayoiomba Kwa Wakati Pamoja na Kupata Taarifa Kwa Kuchelewa Juu ya Maonyesho ya Bidhaa Zao Sehemu Mbalimbali Hasa Nje ya Mkoa wa Njombe. Aidha Katibu Huyo Ameiomba Serikali Kuyawezesha Kiuchumi Mashrika na Taasisi Ambazo ni Changa Zenye Lengo la Kuwawezesha Wananchi Hususani Wanawake na Vijana Ili Kuweza Kujiajiri Wenyewe na Kuacha Kutegemea Ajira Serikalini. Shirika la Wanawake Molimoli Lilianzishwa Mwaka 1994 Ambalo Linajishughulisha na Masuala ya Utunzaji wa Mazingira,Utoaji Elimu Juu ya Ujasiriamali na Kuwasaidia Watoto Wanaoishi Katika Mazingira Magumu. .....................................................................................

0 comments:

Post a Comment