NJOMBE
Mtoto Mmoja Anayekadiriwa Kuwa na Umri wa Miezi Minne wa Jinsia ya Kike Ameokotwa Jana Akiwa Ametupwa na Mtu Asiyejulikana Kandokando ya Dimbwi la Maji Machafu Kwenye Mstu Uliopo Karibu na Shule ya Sekonadari ya Njombe .
Akizungumza na kituo hiki mara baada ya kuokotwa kwa mtoto huyo na wasamalia wema Afisa mtendaji wa kata ya Njombe Mjini Dornad Mng'ong'o amesema kuwa mtoto huyo ameokotwa katika msitu uliopo jirani na shule ya sekondari Njombe akiwa na hali mbaya kandokando ya dimbwi la maji machafu.
Aidha ameeleza kuwa mpaka sasa mtoto huyo yupo chini ya uongozi wa serikali ya mtaa wa Kihesa sehemu ambayo alitupwa.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Kihesa Mjini Njombe Marry Mng'ong'o Ambaye Amemchukua Mtoto Huyo Ameeleza kuwa mtoto huyo amemchukua Jana asubuhi wakati akielekea kwenye ofisi za kata hiyo kwa ajili ya kikao cha sensa kwa viongozi ngazi ya kata na mitaa.