Mwili wa mwanahabari Daud Mwangosi ukiwa chini
Hapa polisi wakiwataka wafuasi wa Chadema kutawanyika eneo la tukio ofisi za Chadema Nyololo Mufindi
Daud Mwangosi kulia enzi za uhai dakika 20 kabla ya kuuwawa kwake
Mwandishi
wa habari wa Chanel Ten mkoa wa Iringa na Mwenyekiti wa chama
chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Daud Mwangosi ameuwawa
katika vurugu za Polisui i na wafuasi wa Chadema katika kijiji cha
Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa leo
Mwanahabari huyo Daud Mwangosi aliuwawa majira ya saa 10 jioni katika
ofisi za Chadema Nyololo huku askari mmoja akijeruhiwa vibaya kwa
risasi .
Kabla ya kuuwawa kwa mwanahabari huyo mabomu yaliweza kupigwa
eneo hilo kuwatawanya wafuasi hao wa Chadema ambao walikuwa
wakigoma kutawanyika eneo hilo na kuamua kukaa chini kuwa hawapo
tayari kuondoka katika ofisi yao.
Chanzo cha mwanahabari Mwangosi kuuawa kilitokana na kukamatwa kwa
mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe mkoa wa Iringa Godfrey
Mushi na hivyo mwanahabari huyo kutaka kuhoji polisi sababu ya
kukamatwa kwa mwanahabari huyo ndipo askari hao walipoanza
kumshambulia kwa kichapo na baadae mlio kama wa bomu ulisikika eneo
hilo na mwandishi huyo na askari mmoja waliaguka chini .
Ndani ya dakika tano ilisikika sauti kutoka kwa askari huyo kuwa
afande nimekufa ndipo walipomchukua na kumpeleka Hospitali ya wilaya
ya Mufindi huku mwili wa mwanahabari huyo ukipelekwa chumba cha
kuhifadhia maiti .
Katika vurugu hizo zilizodumu kwa takribani dakika 30 kwa askari na
wafuasi wa Chadema kurushiana mawe kwa mabomu zaidi ya magari matano
ya Chadema na ya wananchi yameharibiwa huku watu kadhaa
wamejeruhiwa na mwanahabari mmoja Godfrey Mushi akijeruhiwa vibaya.
Hii ni taarifa ya Jeshi la polisi kabla ya tukio kwa vyombo vya habari
JESHI la polisi mkoa wa Iringa limesema limezuia mikutano ya vyama
vya siasa kwa vyama vyote na sio kwa chama cha Demokrasia na
maendeleo (CHADEMA) pekee hivyo laonya vyama vyote kutii sheria bila
shuruti.
Hata hivyo jeshi hilo la Polisi limesema kuwa halifanyi kazi kwa
matakwa ya chama chochote cha siasa na kuwa si kweli kama wanavyodai
viongozi wa Chadema kuwa jeshi la polisi linatumiwa na chama cha
mapinduzi (CCM) kuzuia mikutano hiyo.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Michael Kamuanda ametoa
kauli hiyo leo ofisini kwake alipozungumza na waandisha wa habari
kuhusu zuio la mkutano wa Chadema uliopangwa kuanza leo katika
wilaya ya Mufindi.
" Nawatangazia wanasiasa na vyama vyote vya siasa pamoja na
wananchi wa mkoa wa Iringa kuwa hakutakuwa na mikutano ya kisiasa
kutokana na shughuli za sensa zinazoendelea ....hivyo basi nawaomba
wananchi wote kutoshiriki mikutano yoyote ya kisiasa itakayoitishwa
na wanasiasa "alisisitiza
Kuwa mikutano hiyo imezuiliwa kwa kipindi hiki cha sensa
kilichoongezwa hadi hapo tamko litakapotolewa tena na msajili wa
vyama vya siasa John Tendwa kama alivyokwisha kutoa tamko la kuzuia
shughuli hizo za vyama vya siasa kwa kipindi hiki cha sensa.
"Wananchi wote wa mkoa wa Iringa mnaombwa kutii sheria bila
shuruti hii ni amri ....nawaombeni sana wananchi kutodanganywa na
wanasiasa kwa kuvunja sheria "aliongeza kamanda huyo wa polisi.
Hata hivyo alisema kuwa kimsingi zoezi la sensa lilipaswa
kuhitimishwa Septemba mosi mwaka huu ila kutokana na serikali
kuongeza muda wa zoezi hilo bado jeshi hilo la polisi linazingatia
maagizo ya Msajili wa vyama vya siasa kama alivyoyatoa kwa jeshi
hilo.
Kamanda Kamuanda alisema kuwa jeshi hilo la polisi wala msajili wa
vyama vya siasa hajazuia vyama vya siasa kuendelea na vikao
vyao vya ndani kwa kipindi hiki na kuwa hata Chadema wakiwa mkoani
Iringa wameendelea kufanya vikao vyao vya ndani katika kata mbali
mbali za mkoa wa Iringa na hakuna mtu aliyewazuia kuendelea
kufanya hivyo.
Majibu ya Dkt Slaa
Wakati jeshi la polisi likipinga shughuli hizo za vyama vya
siasa kufanya mikutano ya hadhara katibu mkuu wa Chadema Taifa Dkt
Willbroad Slaa ameibuka na kusema kuwa chama chake kitaendelea
na mikutano kama kilivyojipangia na kuwa wapo tayari kwa lolote
litakalojitokeza .
Dkt Slaa alisema kuwa walivumilia mara ya kwanza walipozuiwa
mikutano hiyo mkoani Iringa na kuvuta subira hadi jumamosi zoezi
hilo lilipomalizika sasa anashangazwa kuona jeshi hilo likiendelea
kuzuia mikutano hiyo tena.
"Tumemsikiliza kamishina wa sensa Hajati Amina Mrisho Said kuwa hadi
sasa watu asilimia 95 wameandikishwa huku akiwata wale ambao bado
kuwapigia simu wenyeviti wa mitaaa na vijiji ili wakaandikishwe
na makarani wa sensa ....sasa jeshi la polisi linataka kutuambia
kuwa hao watu asilimia 5 waliobaki wapo Iringa peke yake hadi
wakazuia mikutano yetu? tunasema hatutakubali tutaendelea na mikutano
yetu kama kawaida hatupotayari kabisa kusubiri hadi tarehe nane"
alisema Dkt Slaa.
Pia alisema kuwa kama ni uzalendo sasa umefika kikomo na kuwa
wataendelea na ratiba zao za mikutano kama ilivyopangwa na
watapambana kwa lolote .
Monday, September 3, 2012
HIVI NDIVYO MWANAHABARI DAUD MWANGOSI ALIVYOPOTEZA MAISHA LEO KATIKA VURUGU ZA CHADEMA NA POLISI
Labels:
Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment